Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A'rafi, Mkurugenzi wa Hawza, ametoa ujumbe wa kutoa pole kufuatia kufariki kwa Ayatullah al-Udhma Fayyadh, mmoja wa Maraji' wa taqlid wa Iraq, Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
إنا لله وإنا إليه راجعون
Imepokewa kutoka kwa Imamu wetu Ja'far Sadiq (as):
اذا مات العالم ثلم فی الاسلام ثلمة لایسدها شیئ الی یوم القیامة
“Anapofariki mwanachuoni, katika Uislamu hutokea pengo ambalo hakuna kitu kitakachoweza kuliziba hadi Siku ya Kiyama.”
Katika siku za mwanzo za Idi Kubwa ya Mwenyezi Mungu, Idi tukufu ya Ghadir na masiku ya kukamilika kwa dini na kutimizwa neema, kupaa kwa kimalaika kwa Marji' mkubwa wa taqlid, Hadhrat Ayatullah al-Udhma Haj Sheikh Muhammad Ishaq Fayyadh (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), kumesababisha huzuni kubwa.
Yeye ambaye alikuwa miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Ayatullah al-Udhma Khui (q.s.), katika maisha yake yenye kheri na baraka hakuwahi kuacha juhudi yoyote katika njia ya kuinua neno la Mwenyezi Mungu na kueneza mafundisho safi ya Ahlul-Bayt wa Ismah na Twahara (as), ameacha nyuma hazina kubwa ya athari za kielimu na kifiqhi ambazo zote ni akiba muhimu kwa Hawza za Kiislamu.
Ubunifu wa kielimu na kifiqhi sambamba na huduma za kidini na tablighi za Marji' huyu mkubwa, hasa mchango wake wa kukumbukwa katika kufufua ibada ya matembezi ya Arubaini na huduma za kijamii na kitamaduni kwa taifa na watu wa Iraq pamoja na Afghanistan, vilimjengea nafasi ya kuwa shakhsia mashuhuri.
Mimi ninatoa pole kwa Imam wa Zama (a.f.), Mar'aji' wakuu wa Taqlid (baraka zao zidumu), hususan Marjaiyya kuu ya Najaf, Hadhrat Ayatullah al-Udhma Sistani (Mwenyezi Mungu adumishe kivuli chake kitukufu), Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Mwenyezi Mungu adumishe utukufu na kivuli chake), Hawza za Najaf, Qum na Afghanistan, Hawza zote za Kiislamu, familia yake tukufu, watoto wake watukufu, wanafunzi wake na wapenzi wa marehemu huyu mwema, na hasa watu pamoja na serikali za nchi mbili rafiki na pendwa za Iraq na Afghanistan.
Pia ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu na kumpa radhi zake Marji' huyu mtukufu, na kwa waliobaki awape subira na malipo mema.
عاش سعیدا و مات سعیدا
“Aliishi hali ya kuwa mwema na akafariki hali ya kuwa mwema.”
Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Kiislamu
Maoni yako